All News and Downloads
TANGAZO LA NAFASI ZA MASOMO 2023/2024Uongozi wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi BWIMA (BWIHAS) kilichopo Jijini MWANZA, unatangaza nafasi za masomo kwa mwaka wa masomo 2023/2024 kwa kozi zifuatazo;
Vigezo vya kujiunga kwa kila kozi ni kama ifuatavyo; Stashahada ya Utabibu mwombaji anatakiwa kuwa amehitimu kidato cha nne na kufaulu angalau masomo manne yasiyo ya dini kwa angalau alama "D" yakiwemo masomo ya Fizikia, Kemia na Baiolojia. Stashahada ya Famasia mwombaji anatakiwa kuwa amehitimu kidato cha nne na kufaulu angalau masomo manne yasiyo ya dini kwa angalau alama "D" yakiwemo masomo ya Kemia na Baiolojia. Stashahada ya Ustawi wa Jamii mwombaji anatakiwa kuwa amehitimu kidato cha nne na kufaulu angalau masomo yoyote manne yasiyo ya dini kwa angalau alama D. Ada zetu ni nafuu na zinalipwa kwa awamu, pia tunatoa huduma ya bweni ambayo inapatikana ndani ya chuo na usafiri wa kwenda kwenye maeneo ya kujifunzia kwa vitendo BURE. Huduma ya chakula pia inapatikana Chuoni kwa gharama nafuu. Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia 0710583683/0767493683/0675988104. Unaweza kutuma maombi kwa kupakua na kujaza fomu ya maombi au BOFYA HAPA KUTUMA MAOMBI MOJA KWA MOJA.
|
|
1. Download Filename-bwihas application form 2023_2024.pdf |